Zelensky anasema anataka kumaliza vita kwa diplomasia
16 Novemba 2024Matarajio ya Trump kurejea madarakani yameibua maswali kuhusu hatma ya mzozo huo, kutokana na Mrepublican huyo kukosoa waziwazi msaada wa kijeshi kwa Kyiv.
Zelensky alizungumzia umuhimu wa diplomasia huku akikataa masharti ya Rais wa Urusi Vladimir Putin ya kuitaka Kyiv kuachia maeneo yalitwaliwa na Urusi.
Soma pia: Zelensky aelezea kusikitishwa na mazungumzo ya Scholz, Putin
Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alifanya mazungumzo ya simu na Putin, licha ya pingamizi kutoka Ukraine, ambayo iliiona hatua hiyo kama jaribio la kumfurahisha Putin.
Soma pia: Tahadhari ya mashambulio ya anga yatolewa kote Ukraine
Wakati mzozo ukiendelea, Zelensky amesisitiza hasara kubwa zinazovikabili vikosi vya Urusi, huku mataifa ya G7 yakirudia msimamo wake wa kuiunga mkono Ukraine, na kuilaumu Urusi kama kikwazo pekee cha amani.